Showing posts with label Katibu Mkuu wa Wizara ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki. Show all posts
Showing posts with label Katibu Mkuu wa Wizara ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki. Show all posts

Friday, October 21, 2016

Waziri Mahiga afungua Mkutano wa Majadiliano ya Amani na Ulinzi kati ya SADC na EU

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Augustine Mahiga akitoa hotuba ya ufunguzi kwenye Mkutano wa majadiliano ya amani na ulinzi kati ya nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) na Umoja wa Ulaya (EU) unaofanyika katika Hoteli ya New Afrika Jijini Dar es Salaam. Pamoja na mambo mengine Mkutano huo unarajia kujadili kuhusu masuala yafuatayo; Aina za chaguzi na jinsi zinavyosimamiwa miongoni mwa nchi wanachama, Vijana wa Afrika wanaokimbilia Ulaya kutafuta maisha, tishio la amani ya Kanda  na Dunia.