Showing posts with label Kaimu Katibu Mkuu wa Chama cha United Democratic Party (UDP). Show all posts
Showing posts with label Kaimu Katibu Mkuu wa Chama cha United Democratic Party (UDP). Show all posts

Friday, July 01, 2016

OFISI YA MSAJILI WA VYAMA VYA SIASA YAENDELEA NA UHAKIKI WA VYAMA NCHINI.

Zoezi la uhakiki wa utekelezaji wa masharti ya usajili wa Vyama va Siasa kwa upande wa Tanzania Bara linaendelea .Tayari vyama 18 vimekwishakuhakikiwa. Vyama vinne vinatarajiwa kuhakikiwa Julai 4. Zoezi hili ni zoezi la kawaida na endelevu ambalo hufanyika kila mwaka ili kupima endapo vyama vya siasa vinakidhi matakwa ya Sheria ya usajili wa vyama vya Siasa.

Uhakiki wa Vyama vya siasa ni zoezi muhimu sana kwa sababu ni zoezi ambalo hugusa uhai wa kila chama cha siasa. Kwa upande wa Tanzania Visiwani , uhakiki unatarajiwa kuanza mara baada ya kumalizika Bara kwa tarehe ambazo zitatangazwa baadaye. 
Esther B.Mwanri, Mwanasheria kutoka Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa akikagua katiba ya Chama cha Wananchi (CUF) wakati wa Zoezi la uhakiki uliofanyika katika ofisi za chama hicho zilizopo Buguruni Malapa Jijini Dar es salaam. Kushoto ni Bw. Shaweji Mketo, Mkurugenzi wa uchumi na Mipango.(Picha zote na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa)