Mahakama ya Hakimu Mkazi Dodoma, ilimhukumu kifungo cha miaka 30, Godfrey Mjelwa (48), baada ya kupatikana na hatia ya kuishi kinyumba na binti yake wa kumzaa.
Hakimu Mkazi katika mahakama hiyo, Mwajuma Lukindo alisema ushahidi wa pande zote ulithibitisha kuwa mtuhumiwa alitenda kosa hilo la kuishi chumba kimoja na binti yake, kama mke na mume.
