Showing posts with label Balozi Mdogo wa Uingereza.. Show all posts
Showing posts with label Balozi Mdogo wa Uingereza.. Show all posts

Thursday, March 10, 2016

MAHAKIMU WAMETAKIWA KUTUMIA TAALUMA VYEMA KATIKA KUAMUA KESI.

 Balozi Mdogo wa Uingereza, Matt Sutherland  akizungumza na wandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusiana na Uingereza na Tanzania kufanya kazi kwa pamoja katika mafunzo haya. Historia yenye kufanana katika sheria na taasisi zetu za kisheria inatoa fursa pana kwa nchi hizi kuweza kufanya kazi na kujifunza baina ya kila mmoja. Mafunzo haya yatawezesha kutoa ujuzi wenye thamani kwa wale watendaji wa mstari wa mbele katika kupambana na makosa makubwa nchini Tanzania.leo jijini Dar es Salaam kushoto ni Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Shaban Lila.
 Jaji Kiongozi kutoka mahakama kuu ya Tanzania Shaban Lila akizungumza na wandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya mahakimu watatumia  ujuzi  na elimu walioipata katika kutatua changamoto ya ucheleweshwaji wa kesi na mashauri mbalimbali, leo jijini Dar es Salaam.
 Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Shaban Lila akimpa cheti chamafunzo ya namna ya kushughulikia makosa makubwa Joachim Tiganga katika hoteli ya White Sands, Mbezi Beach, Dar es Salaam.