Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji Muhandisi Mbogo Futakamba akibonyeza moja ya mashine inayoongoza pampu za kusukuma Majikwenda jijini Dar es salaam kutoka Mtambo wa kuzalisha Maji wa Ruvu Chini wilayani Bagamoyo mkoani Pwani ikiwa ni sehemu ya majaribio ya mtambo huomara baada kukamilika kwa ujenzi wa bomba la kusafirisha maji lenye urefu
wa kilometa 55.9.
Mkuu wa Matengenezo wa Mtambo wa kuzalisha maji wa Ruvu Chini Tumaini Ndosi (aliyepanda juu) akitoa ufafanuzi kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji Muhandisi Mbogo Futakamba kuhusu moja ya mita inayosoma kiwango cha ujazo wa maji yanayosafirishwa kutoka kwenye Pampu za kusukumia maji.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji Muhandisi Mbogo Futakamba (kulia) akizungumza jambo na Meneja wa Mtambo wa kuzalisha maji wa Ruvu Chini, Emmanuel Makusa (kushoto) na Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASCO Muhandisi Cyprian Luhemeja mara baada ya kukagua mitambo na pampu za kusukumia Maji za Mtambo wa Ruvu Chini, Bagamoyo mkoani Pwani.