Friday, June 23, 2017

KUTOKA SHIMONI KABLA HUJAFA.

Watanzania wametakiwa kusimama katika zamu na nafasi zao ili waweze kutolewa katika mashimo walikowekwa.
Kauli hiyo imetolewa na mwinjilisti wa kimataifa George banali wakati akihubiri katika viwanja vya wapo mission International vilivyoko mbezi Beach Jogoo jijini Dar es salaam,ambapo alisema kuwa njia pekee ya mtanzania kufanikiwa kutoa katika shimo la mateso ni kumpa Yesu maisha yake.
Aidha alisema kuwa kutokana na watu wengi kuendelea kuteseka na kutaabika njia moja tu ni kumpokea bwana Yesu kama Bwana na Mwokozi wa maisha yako na hautaendeleea kukaa katika shimo.
Inawezekana shilo ulilowekwa ni shimo la mateso magonjwa na shida mbalimbali pamoja na kuonewa na nguvu za giza sasa ni wakati wako wa kufunguliwa na kuwekwa huru katika maisha yako.
Mukutano huo bado unaendelea ambapo waimbaji mbalimbali wa nyimbo za injili wanahudumu kama vile Yes Kwaya,faraja Ntaboba,kikundi cha kusifu na kuabudu cha BCIC na waimbaji wengine wengi.